business/biashara

Gharama ya riba za kigeni hupanda kwa shilingi bilioni .14.5 mwisho wa kusitishwa kwa malipo ya deni

Gharama za riba za kigeni za Kenya zilipanda kwa shilingi bilioni 14.5 bilioni hadi shilingi bilioni 120.8 katika mwaka wa fedha uliohitimishwa wa 2021-2022 mwishoni mwa mpango wa kusimamisha huduma ya deni (DSSI).

Kulingana na data kutoka kwa Hazina ya Kitaifa, gharama za riba kutoka nje zilipanda kutoka shilingi bilioni .106.3 wakati dirisha la DSSI lilipofungwa mnamo Desemba 2021.

Mpango wa DSSI ulianza Juni 2020 na baadaye ulipanuliwa hadi kufikia 2021, na kuruhusu nchi zinazoendelea kusitisha malipo ya deni la nje.

Hata hivyo Kenya ilichelewa kushiriki na kujiunga na mpango wa DSSI miezi sita baadaye Januari mwaka jana.

Ufichuzi wa awali wa Hazina ya Kitaifa kwa Hazina ya Kimataifa ya Fedha (IMF) unaonyesha Kenya iliokoa wastani wa shilingi bilioni .60.3 sawa na (dollar milioni 503.8) kutoka kwa ushiriki wa DSSI.

Akiba kutoka kwa DSSI ilipungua kwa kasi katika nusu ya pili ya mwaka hadi shilingi bilioni .9.6  sawa na  (dola milioni 80.3) kwani wakopeshaji wa Kenya wasio wa Paris kama vile Uchina waliondoa uungwaji mkono wao kutoka kwa mpango huo.

Kwa jumla, Kenya ilitumia shilingi bilioni 577.6 kwa malipo ya riba ya deni katika mwaka wa kifedha wa 2021-2022, ongezeko la asilimia 16.7 kutoka shilingi bilioni .495.1 hapo awali.

Wakati uo huo, malipo ya riba ya ndani yaliongezeka kwa asilimia 17.5 hadi shilingi bilioni 456.8 kutoka shilingi bilioni .388.8 Juni 2021.

Jumla ya malipo ya riba yalifikia asilimia 19.12 ya jumla ya matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2021-22.

About the author

admin

Leave a Comment