Wakati tu Malkia amefariki dunia, kiti cha enzi kinapitishwa mara moja bila sherehe yoyote kwa mrithi, Charles, Mkuu wa zamani wa Wales.
Lakini kuna hatua kadhaa za kiutendaji – na za kitamaduni ambazo lazima azipitie ili kutawazwa kuwa Mfalme.
Moja kati ya vitu vya kwanza atakavyofanya ni kuamua kama atatawala kama Mfalme Charles wa tatu au kuchukua jina lingine.
Kwa mfano, jina la babu yake George wa tano lilikuwa Albert, lakini alitawala kwa kutumia mojawapo ya majina yake ya kati.
Charles anaweza kuchagua kutoka kwa mojawapo ya majina yake manne – Charles Philip Arthur George.
Ingawa yeye ndiye mrithi wa kiti cha enzi, Prince William hatakuwa Mkuu wa Wales moja kwa moja.
Hata hivyo, moja kwa moja anarithi jina lingine la baba yake, Duke of Cornwall.
Mkewe Catherine atajulikana kama Duchess of Cornwall.
Pia kutakuwa na jina jipya la mke wa Charles, ambaye majina yake kamili yatakuwa Malkia Consort – neno linalotumiwa kwa mwenzi wa mfalme.
Katika muda wa saa 24 au zaidi baada ya kifo cha mamake, Charles atatangazwa rasmi kuwa Mfalme.
Hii itafanyika katika kasri la St James’s huko London, mbele ya baraza la sherehe linalojulikana kama Baraza la kukabidhi Mamlaka.
Leave a Comment