Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania imesema kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kwamba kumejitokeza mlipuko wa ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, Jimbo la Tshopo, ambapo Watu 261 wameugua na 129 kufariki.
Wizara ya Afya Tanzania imewataka Watanzania
kuchukua tahadhari kwani magonjwa hayana mipaka hususani mikoa inayopakana na
DRC.
Dalili kuu za ugonjwa huu ni homa kali, kichwa
kuuma, kutapika, kuogopa mwanga, kuchanganyikiwa na shingo kukakamaa.
Ugonjwa huu unaweza kusababisha madhara makubwa
kwenye ubongo, kupotea kwa usikivu au ulemavu mwingine wa kudumu na hata
kupoteza maisha
Ugonjwa huu husababishwa na vinkers aina ya bakteria
wanaojulikana kama Neisseria Meningitids na huambukizwa kutoka Mtu mmoja kwenda
kwa mwingine kwa njia ya hewa au kukaa na Mtu mwenye maambukizi na huchukua
siku 2 hadi 10 tangu kuambukizwa hadi kuanza kuonesha dalili
Watu wanahimizwa kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima watu
wengi.
Leave a Comment