International

KIMATAIFA: UTAMUUTAMU KWA KENYA NA MISRI!!!

Written by admin

Kenya na Misri ni miongoni mwa nchi nane ambazo, leo Jumatano, zimeondolewa kwenye orodha ya mataifa yaliyopigwa marufuku kuingia Uingereza wakati serikali ya nchi hiyo inapoanza kutekeleza mabadiliko kwenye mfumo wake wenye utata wa usafiri kimataifa.

Habari hii imepokelewa kama
afueni kubwa humu nchini ambapo sekta ya utalii imepata hasara kubwa kufuatia
vizuizi vya usafiri kama njia moja ya kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19.

Uingereza ni ya nne yenye mchango mkubwa zaidi kwa watalii wanaotembelea Kenya ambapo kwa sasa hivi ipo katikati ya msimu wake wa kilele cha utalii ambao unamalizika na uhamiaji wa nyumbu kila mwaka.

Furaha ya kukaribisha zaidi ya
watalii 100 waliowasili katika uwanja wa ndege wa Mombasa, zimeshuhudiwa kwa
mbwembwe na taadhima kuu.

Wageni waliowasili ni wa
Romania ambao ni watalii wapya katika soko la Kenya.

About the author

admin

Leave a Comment