Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In amesema kuwa mda sahihi umefika wa kupiga marufuku ulaji wa mbwa katika nchi hiyo.
Rais Moon ambaye ni mmoja wa watu wanaopenda ufugaji wa mbwa alisema upigaji marufuku wa ulaji wa mbwa ni njia mojawapo itakayosaidia kulinda wanyama hao wasitokomee zaidi.
Waaidha, inasemekana kuwa ulaji wa nyama ya mbwa umeshuka ingawa bado mbwa milioni takribani moja huchinjwa kwa mwaka.
Nchi ya Korea Kusini tayari imepiga marufuku uchinjani wa kikatili wa mbwa na paka ila ulaji wa nyama hizo haukuwahi kupigwa marufuku.
Leave a Comment