Music/Miziki

Esma Platnumz: Natafuta mchumba mwenye macho mazuri kama ya kakangu Diamond

mawafi
Written by admin

Dadake msanii namba moja wa muda wote katika ukanda wa Afrika Mashariki, Diamond Platnumz, Esma Khan ama Esma Platnumz kama anavyojulikana na wengi kwa mara nyingine ameibuka na utani kwa kina dada kuwa anatafuta mchumba.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Esma Platnumz alipakia picha ya ndugu yake Diamond Platnumz ambaye ni mdogo wake na kusema kwamba anatafuta mchumba mwenye macho mazuri kama ya ndugu yake Diamond Platnumz.

Pia alidokeza kwamba wamekawia sana kumuona wifi wao tena na kusema wifi wao ambao ni mke atakayeolewa na Diamond ana kila haki la kulia pamoja pia na kuimbiwa nyimbo ambazo alizitaja kama za uongo na baadhi za ukweli kutoka kwa msanii huyo.

 “Nyie natafuta Mchumba mwenye macho Mazuriiii kama ya mdogo wangu NASEEB. Mawifi zangu wana haki ya kulialia pamoja pia na kuimbiwa nyimbo za uongo na kweli ” Esma aliandika kwenye picha hiyo.

Esma hajakuwa mwenye bahati katika mapenzi kwani ndoa yake ilisambaratika awali na baadae uhusiano wake mwingine tena ukavunjika. Ni kama sasa hivi tena amepona na yupo sokoni anataka kujaribu bahati tena.

Watumizi wa mtandao wa Instagram walitolea maoni yao tofauti tofauti huku wengine wakisema Diamond hawezi kosa mwanamke wa kumuoa hata kama atajua anamwimbia uongo kwani ni pesa na umaarufu tu wanatafuta kwa sababu macho kutoka zamani msanii huyo anayo.

About the author

admin

Leave a Comment