Mchekeshaji na mwandishi mashuhuri Eddie Butita amedokeza kuwa huenda akaitwa baba hivi karibuni.
Alhamisi, mchekeshaji huyo wa zamani wa Churchill Show alichapisha video iliyoonyesha akimpapasa mjamzito na kuambatanisha na ujumbe ulioashiria kuwa ni mtoto wake aliyebebwa tumboni.
“Ni mvulana au ni msichana? Jumatatu 9.00AM #TheGrandGenderReveal,” aliandika kwenye video hiyo.
Butita aliambatanisha video hiyo na wimbo wa Nadia Mukami na Arrow Bwoy ‘Kai Wangu’ ambao walimwimbia mtoto wao.
Katika maelezo ya video hiyo, mchekeshaji huyo alidokeza kwamba anafurahi sana kuhusu ujauzito huo.
“Hakuna maneno yanaweza kuelezea hili, 2 imekuwa nambari yangu ya bahati kila wakati na 2022 ina mbili tatu. Ni mvulana au msichana? Tuonane Jumatatu,” aliandika.
Hata kabla ya madai ya Butita kuthibitishwa kuwa kweli ama kiki tu, Wanamitandao Wakenya wakiwemo watu kadhaa mashuhuri walikuwa wepesi kumpongeza mchekeshaji huyo kwa hatua hiyo kubwa.
Hata hivyo, baadhi walieleza mashaka yao kuhusu madai ya msanii huyo na kusema kwamba alikuwa akiigiza tu.
Blessednjugush: Hongera kwa booties
jackyvike: Ala ulienda kugawa nyota, nyota nayo ikagawana, kongole
ogaobinna: Hiyo nitumbo ya dem ya wenyewe unashika hivyo
mcatricky: We wacha kutuenjoy
celestinendinda: Hongera kwa Butitas
dj shiti_comedian: Pongezi sana CEO
Leave a Comment