Wanandoa mashuhuri Blessed Njugush na Celestine Ndinda wametangaza kuzaliwa kwa mtoto wao wa pili.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Bi Ndinda alifichua kuwa mwanao Toria alizaliwa mwezi mmoja uliopita.
“Ni mwezi mmoja sasa tangu tulipokaribisha mwanachama mpya wa familia yetu, Baby Toria. Shukran kwa maombi na jumbe za kheri njema,” alitangaza siku ya Jumamosi.
Aliongeza “Mama Boys, Tugi & Toria (inyaa tuvisi).”
Wanandoa hao walikuwa wameziweka siri habari kuhusu mtoto wao tangu kuzaliwa kwake mwezi uliopita.
Wanamitandao wakiwemo watu mashuhuri walifurika chini ya ujumbe huo kuwapongeza kwa zawadi ya mtoto.
Kabiwajesus Hongera ?
Bettymuteikyallo Hongera Ndinda. Familia yako ibarikiwe. Najua Tugi amefurahi! Muwe sawa.❤
Kalekyemumo Awww Hongera inyaa tuvisi ????
Milly Chebby Hongera Mama Boys
giladmillo ❤❤❤
Habari kuhusu ujauzito wa pili wa Bi Ndinda na mumewe Njugush zilikuja kufichuka takriban miezi mitano iliyopita wakati wa tamasha lao la TTT3 ambalo waliandaa katika ukumbi wa Nairobi Cinema.
Wanandoa hao ambao pia ni waigizaji wenza wamekuwa katika ndoa kwa takriban miaka sita na tayari wana mtoto mwingine mmoja wa kiume pamoja, Tugi ambaye alizaliwa mnamo mwezi Machi, 2018.
Wawili hao walifunga pingu za maisha mwezi Desemba 2016 na wakagundua ujauzito wa mtoto wao wa kwanza takriban miezi minne baadae.
Leave a Comment