Music/Miziki

Mapenzi tele, Kennedy Rapudo amsifia mpenzi wake Amber Ray siku ya kuzaliwa

Written by admin

Mpenziwe mwanasholaiti Amber Ray, Kennedy Rapudo alimwandikia ujumbe mtamu huku akimtakia heri njema ya kuzaliwa.

Rapudo alimwandalia Amber sherehe ya kipekee ya kuzaliwa kwake na kumwonyesha mpenzi wake upendo siku ya Alhamisi.

Katika Instastory zake alipakia video na kumwandikia Amber na kusema kuwa anatumai kuwa naye maishani.

 “Heri ya kuzaliwa kwa mwenzangu wa roho, mpenzi wangu na rafiki yangu bora. Daima tuone usiku na mchana pamoja! Heri njema kwa siku ya kuzaliwa HER grace, “Rapudo aliandika huku akionyesha maua.

Video hiyo ilikuwa na maua ya waridi yaliyopangwa kwa ustaarabu kuonyesha  jina la AMBER na mishumaa kupangwa kando.

Rapudo alipakia picha na video zingine za sherehe hiyo aliyokuwa imenoga.

Aliendelea kumsifia na kumtakia mema kwa siku yake ya kuzaliwa na hata baada ya siku hiyo.

“Heri ya kuzaliwa msichana ambaye ana sifa za kuwa mke wangu. Nakutakia neema na fanaka kwa siku yako. Nimebarikiwa sana kuwa nawe,” Rapudo alisema.

Zaidi ya hayo Rapudo bado alipakia picha ya Amber Ray katika ukurasa wake wa Instagram kisha kumwandikia ujumbe mwengine.

“Mpenzi wangu, sijawahi kuwa na furaha hadi pale ulipokuwa maishani mwangu. Wewe ni mtu ninaemthamini sana. Katika siku yako hii maalum, ninakuombea mema katika maisha yako, upendo, amani na furaha katika maisha yako. Mungu akufunike kwa upendo wake wa kipekee na akumiminie baraka zake tele. Happy birthday baby love,” Rapudo alisema.

 Amber Ray alimshukuru mpenzi wake kwa hayo yote na kwa kumzawadi sherehe.

“Kennedy Rapudo asante sana mpenzi wangu. Nina furaha kuwa sikukata tamaa kwa mapenzi. Nakupenda,” Amber alisema.

Mapenzi yao yamekuwa yakinoga baada ya wawili hao kuwafahamisha wazazi wao kuwa wanachumbiana.

About the author

admin

Leave a Comment