Music/Miziki

MAPENZI YANA-RUN DUNIA

MAPENZI KONKI LIQUID
Written by admin

Mwanamuziki nyota kutoka taifa jirani la Tanzania Rajab Abdul Kahali maarufu kama Harmonize huenda amebadili dini baada ya kuzama katika mapenzi na mcheza filamu Frida Kajala.

Harmonize Muislamu na Kajala Mkristo


Harmonize ni Muislamu kinda kindaki tangu utotoni na alizaliwa katika familia ya Kiislamu huku mpenzi wake Kajala akiwa ni wa dini ya Kikristo.

Suala la dini bila shaka huwa kigezo katika ndoa na baada ya wawili hao kuvishana pete za uchumba, maswali yalikuwa mengi kuhusu mustakabali wa dini ya kila mmoja.


Lakini licha ya wengi kuibua maswali kuhusu utata wa dini inaozingira wachuma hao, Harmonize aliweka wazi kuwa hatampa mpenzi wake masharti ya kubadili dini yake ili kuwa mke wake.

Harmonize ndiye anayeonekana kubadili dini
Na ilivyo katika ulimwengu, uwezo wa mwanamke katika mapenzi ni mkubwa sasa kiasi cha kuamua mawimbi ya dunia, msanii Ali Kiba aliwahi kuimba katika wimbo wake wa Mapenzi Yanarun Dunia.

Ilivyo kwa sasa inaoneka Kajala ndiye amefanikiwa kumshawishi Harmonize kubadili dini yake penzi lao linapozidi kunoga – kutoka kwa Uislamu kwenda kwa Ukristo.

Jumapili, Septemba 11, wapenzi hao walioneka wakiwa wamevalia mavazi rasmi na ya heshima na kuwa eneo linalooneka kuwa kama kanisa.

Kupitia kwenye Instastories, Kajala alipakia wimbo akicheza na Harmonize na kuambatanisha na maneneo yanayoashiria kuwa ilikuwa ibaada kanisani.

“Baada ya kutoka kanisani mimi na kijana wangu,” Kajala aliandika kwenye video hiyo naye Harmonize akajibu: “Mashallah mtoto wa kisukuma, ahsante kwa kumfanya kijana mtoro kung’aa tena.”

About the author

admin

Leave a Comment