Sosholaiti Vera Sidika amefichua kwamba alianza kutumia dawa za kupanga uzazi kitambo sana, alipokuwa angali chuoni, zilizochangia kuwa na makalio makubwa kupita kiasi.
Vera alisimulia jinsi alivyokuwa akidungwa sindano kila miezi mitatu na kuzoea hivyo hata wakati hakuwa kwenye mahusiano.
Vera alisema sindano hizo za kupanga uzazi zilimsababisha kukosa hedhi. “Niliendelea kudungwa sindano hiyo hadi nikagundua kwamba nimeongeza uzani, ila nilikuwa na makalio kama unavyyona kwenye picha yangu ya kitambo. Dawa za kupanga uzazi ziliharibu mambo.
Vera Sidika asema hapendi kuwa na makalio makubwa Mama huyo wa mtoto mmoja alisema kwamba hapendi kuwa na makalio makubwa, ingekuwa ni kupenda kwake angeweza kuyapunguza kidogo tu. Sosholaiti huyo ambaye amegeukia usanii alisema kwamba, angefurahia iwapo angekuwa na makalio saizi ya wastani. “Kusema ukweli sipendi makalio yangu. Sikutaka yawe makubwa kiwango hiki. Kama ingekuwa ni uwezo wangu ningeyapunguza yawe madogo, ila sio sana,” Vera aliongeza kusema.
Leave a Comment