Watu 15 wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kamwaura Kuresoi Kusini wakituhumiwa makosa ya kukeketa wasichana wadogo na pia wanawake.
Akidhibitisha kisa hicho kamishna msaidizi wa Keringet Bethsheba Osiemo amesema wakazi wa kijiji cha Kipnanda ndio walimjuza chifu wao David Busienei ya kwamba ukeketaji huo ulikuwa unatekelezewa nyumbani kwa Alice Chumbin, ambapo baadhi ya watu ambao wameshikwa ni walimu wawili pamoja na watu wanne wa familia moja.
Osiemo amekiri visa vya ukeketaji bado vinaendelea kushuhudiwa eneo hilo huku vikiendelezwa faraghani.
Kumi na tano hao wanatarajiwa kufikishwa mbele ya mahakama ya Molo, huku onyo kali likitolewa kwa wale wanaoendeleza mila na tamaduni ambazo zimepitwa na wakati.
Leave a Comment