News

Afueni kwa wakaazi wa Molo

Written by admin

Katika eneo la Molo ni visa vitatu  ambavyo vimeripotiwa vya dalili za Covid-19 lakini vyote zimedhibitishwa kuwa nje ya hatari ya virusi hivyo.

Naibu Kamishina wa kaunti ndogo ya Molo David Wanyonyi amesema idara ya usalama pamoja na ile ya afya zinafanya kazi bega kwa bega ili kuhakikisha eneo hilo liko salama

Akiongea katika kikao na wanahabari Wanyonyi amesema serikali inaendelea kuratibu mipango ya kukabiliana na virusi vya covid-19

Huku hayo yakijiri…

Makao ya wazee mjini Nakuru yamechukua tahadhari mapema ya kuwakinga wazee  dhidi ya homa hatari ya corona..Sarah Nyangeri ameongea na meneja msimamizi  katika makao hayo na kuandaa ripoti ifuatayo

Usimamizi wa makao ya wazee  mjini Nakuru umepiga marufuku wageni kwenye  makao ya wakongwe hao  sawa na kuzuia wazee hao kuondoka makaoni  wakisema ni kwenye juhudi za kuzuia maambukizi ya homa ya corona.

Monica wanjiku ni Meneja msimamizi wa makao hayo viungani mwa mji wa Nakuru na  amesema kuwa hatua hiyoni bora kuwazuia wazee hao dhidi ya homa hiyo angamizi ya  corona.

Aidha, amesema kuwa wazee hao hawaruhusiwi kutoka kwenye makao hayo kutafuta huduma za afya akidokeza kuwa  mikakati imewekwa ya kuwahudumia kikamilifu.

Kwa upande wa Wazee hao hofu yao kuu ikiwa maambukizi  ya homa hiyo wakizingatia umri wao wa  miaka sitini  na kwenda juu na  ambao umetajwa kuwa hatari kwa janga hilo la covid 19.

Sarah Nyangeri

About the author

admin

Leave a Comment