News/Habari

Ajali yakatiza maisha ya 2 papohapo

Written by admin

Watu wawili wamefariki baada ya kuhusika kwenye ajali katika eneo la Migaa kule Rongai barabara kuu ya Nakuru kuelekea Eldoret asubuhi ya leo.

Ajali hiyo imetokea baada ya breki za lori hilo kufeli na kugongana ana kwa ana na trela. Lori hilo aina ya Canter lilikuwa likisafirisha mahindi kutoka Uganda kuja humu nchini.

Utingo wa lori hilo aliyejitambua kama Osman Kilochi amesema kwamba dereva alijaribu mara kadhaa kulidhibiti bila  mafanikio baada ya breki zake kufeli.

Gari la kuzima moto kutoka kaunti ndogo ya Molo pia lilihusika kwenye ajali hiyo, kulingana na mwakilishi wadi mteule kwenye bunge la kaunti ya Nakuru Rachael Maru.

Miili ya marehemu imepelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti mjini Nakuru.

About the author

admin

Leave a Comment