Jambazi mmoja amepigwa na wananchi hadi kufa, mwingine akiponea kifo baada yao kupatikana wakijaribu kumpokonya mwanamke mmoja pesa katika barabara kuu ya Eldoret kuelekea Uganda karibu na kanisa la IVC viungani mwa mji wa Eldoret.
Akithibitisha hayo mkuu wa polisi eneo la Eldoret Magharibi Eliud Maiyo, anasema majambazi hao watatu walikuwa wamejihami kwa bastola bandia na walikuwa na pikipiki tayari kupora na kutoroka.
Maiyo amesema huku mmoja wa majambazi hao akiokolewa na maafisa wa polisi, jambazi wa tatu alifanikiwa kutoroka.
Mwili wa jambazi huyo mwenye umri wa miaka 25 umehifadhiwa Katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya rufaa na mafunzo ya Moi Eldoret,huku mwenzake wa miaka 35 akisalia korokoroni Katika Kituo cha polisi Cha Central Eldoret baada ya kupokea matibabu.
JUDY CHERONO
Leave a Comment