News/Habari

Bado hujafikiwa-Daddy Owen amjibu Pritty Vishy

Written by admin

Mshawishi wa mitandao ya kijamii Pritty Vishy, ​​ambaye jina lake halisi ni Purity Vishenwa, amejitolea kuwa mke kienyeji wa Mwimbaji wa nyimbo za Injili Daddy Owen.

Hii ni baada ya msanii huyo hivi majuzi kutangaza kuwa anatafuta mwanamke wa kumuoa na kusema kwamba kigezo kikubwa ni mwanadada huyo kuwa wa kutoka mashambani na wala si wa mjini.

Vishy ambaye anajiita malkia wa kutoka mashambani ametoa ombi kwa watu wanaoweza kumfikia msanii huyo kumwambia kwamba yupo radhi kuwa mke wake kwani tayari kigezo cha kuwa kienyeji tayari anacho.

Huku msanii huyo akijibu ambi la Vishhy alimwambia kwwamba anapaswa kusubiri kwani foleni ni ndefu sana na kuwa bado hajafikiwa.

“Huyu mwambieni line ni ndeefu,hajafikiwa bado..lakini kama marathon tutazawadi kila mmoja atakaye vuka laini,” Alisema.

Pritty alikua maarufu katika duru za burudani kufuatia uhusiano wake na mwanamuziki Stivo Simple Boy.

Description: https://lh3.googleusercontent.com/6REiJlWScMvV5BidsP1cxLUDY_fetMWr57gnLocjSUkygqTccktUlnyRICSjJgsLX11b31d8g4urlAElVzlweJQ_EGMEVtfeF4ySOYGq3VV5k4E=s567

Daddy Owen, 40, alikuwa amefichua kuwa alikuwa kwenye shinikizo la kuoa tena.

“Natafuta mwanamke wa dhati wa kuchumbiana naye na kuoa. Natafuta mwanamke mwenye ngozi nyeusi, mwenye maombi sana. Anapaswa kuwa kutoka kijijini,” alisema.

Daddy Owen, aliyezaliwa kama Owen Mwatia, alisisitiza: “Ndiyo sababu mimi hutembelea mara kwa mara na kuendesha miradi kijijini. Nataka kupata mwanamke kutoka huko. Sitaki kuchumbiana na mtu aliyezaliwa mjini.”

About the author

admin

Leave a Comment