Operesheni ya kuwakamata wale wanaokiuka sheria katika uuzaji wa vileo ulianza leo katika kaunti ndogo ya Koibatek kaunti ya Baringo.
Kulingana na kamishna wa kaunti ya Baringo Henry Wafula, lengo lao ni kutokomeza uuzaji wa pombe haramu, katika kaunti ya Baringo.
Akizungumza na wanahanari mjini Eldama Ravine, Wafula aliwahimiza wakaazi kufuata kanuni zote za serikali katika uuzaji wa vileo.
Katika oparesheni hiyo wanabiashara wawili walitiwa mbaroni kwa tuhuma za kuvunja sheria ya kuuza vileo.
Leave a Comment