Mwanafunzi mmoja wa miaka 24 katika chuo kikuu cha Bomet amepoteza maisha yake baada ya kuzama katika Chemchemi ya Maji ya Kimaya kwenye Mto Chepkulo.
Akithibitisha kisa hicho, Mkuu wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Chepalungu, Nelson Masai alisema mwanafunzi huyo wa kiume wa mwaka wa pili alikuwa amezuru eneo hilo pamoja na marafiki zake wengine 12.
Masai aliongezea kuwa marehemu pamoja na wenzake huenda walipuuza kina cha mto huo na kuamua kujiharatisha.
Mkuu huyo wa polisi alisema wanafunzi ambao walikuwa wameandamana na marehemu bado hawajatambuliwa lakini wanasakwa na polisi kuandikisha taarifa.
Mwili wa mwanafunzi huyo haujapatikana, kufikia kwa taarifa hii, licha ya msako wa wapiga mbizi wa Bomet kutafuta kila mahali.
Leave a Comment