News/Habari

BUNGOMA :Linda mama mashakani

Written by admin

Hata baada ya rais Uhuru Kenyatta kuzindua mpango wa linda mama, kina mama wengi wajawazito wangali wanapoteza maisha yao kwa kukosa ufahamu kuhusu mpango huo.

Kulingana na Rebeka Masibayi kiongozi wa chama cha kupigania maslahi ya watoto wasichana kaunti ya Bungoma almaarufu Girl Child Advocacy suala hilo limechochewa na idadi kubwa ya kina mama kukosa ufahamu kuhusu mpango wa linda mama.  

Masibayi ametoa changamoto kwa serikali kufanya hamasisho kote nchini kama njia moja ya kuimarisha huduma za linda mama.

“Ombi langu ni serikali iangalie jambo hili kwa kina ili kina mama wasaidike na mpango huu wa Inua mama.”Alisema Rebeka

Na Evans Wamalwa

About the author

admin

Leave a Comment