News/Habari

Chebukati Amshukuru Mkewe, Wanawe kwa Kumpepea Joto la Uchaguzi Lilipozidi

FAMILIA MUHUMI
Written by admin

Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC Wafula Chebukati ameisifia familia yake kwa kusimama na yeye tisti katika kipindi cha uchaguzi mkuu licha ya mawimbi makali kuibuka katika tume hiyo.

Chebukati amemshukuru mkewe Mary na wanawe watatu kwa kusimama naye katika maombi, kitu ambacho amesema kilimpa nguvu na ujasiri wa kufanya kazi yake pasi na kuyumbishwa kwa njia yoyote ile na baadhi ya watu waliotaka atoe matokeo ya uchaguzi kwa upendeleo wao.

Kando na mkewe na wanawe, Chebukati pia amewatambua wazazi wake na ukoo mzima wa familia kwa kusimama naye kipindi hicho kilichokuwa kigumu baada ya makamishna wanne wakiongozwa na naibu mwenyekiti Juliana Cherera kuiasi tume na kujitenga na matokeo ambayo Chebukati alikuwa anatarajiwa kutangaza.

Pia amewatambua na kuwashukuru makamishna waliosimama naye baada ya lile Sakata la Agosti 15 ka kuwataja kama wajasiri ambao nchi hii itawakumbuka milele kama waliosimamia haki licha ya majaribio mengi ya kubuniwa.

Vile vile amemshukuru rais William Ruto kwa kuitambua tume hiyo kama moja ambayo ilijiboreshea pointi katika dunia nzima kwa kuendesha uchaguzi ambao haukuvuja hata kidogo.

Jana baada ya kuapishwa kama rais wa 5, Ruto aliitambua tume ya IEBC ikiongozwa na Chebukati na kusema makamishna waliostahimili vitisho ndio mashujaa wa mchakato wa uchaguzi wa mwaka huu.

About the author

admin

Leave a Comment