News

Chemchemi za maji zazidi kulindwa Mau

Written by admin

Katibu mkuu katika wizara ya mazingira kwenye kaunti ya Nakuru Kiogora Muriithi,amesema kwamba, washikadau mbali mbali kwenye sekta ya mazingira wanaendelea kuweka juhudi za kuboresha na kulinda chemichemi ya maji ya Enapuiyapai katika msitu wa Mau,kama njia moja ya kuendelea kuwavutia watalii nchini.

Akizungumza katika eneo la Kwokwomoi,Muriithi amesema kwamba,chemichemi hiyo imekuwa ikisaida pakubwa katika kusafisha maji ya mto Molo Rongai na pia mto Mara.

Kulingana na kiongozi huyo serikali ya kaunti ya Nakuru inaendelea kuhamasisha wakaazi walioko karibu, kuhusu umuhimu wa chemichemi hiyo na kutenga fedha ambazo zitatumika kuilinda.

About the author

admin

Leave a Comment