Kuna haja ya wanaume na akina mama kuhamasishwa zaidi ili kushiriki vita dhidi ya ukeketaji miongoni mwa akina mama na wasichana humu nchini.
Haya ni kwa mujibu wa mwakilishi wa kina mama kutoka kaunti ya Kirinyaga Wangui Ngirici ambaye amesema kuwa ukeketaji ni dhulma potovu iliyopitwa na wakati.
Akiongea mjini Iten kaunti ndogo ya Keiyo Kaskazini kaunti ya Elgeyo Marakwet mwakilishi huyo amedokeza kuwa ukeketaji wa wasichana umerudisha nyuma nchi kimaendeleo.
Hata hivyo Ngirici amesema kuwa atashirikiana na serikali ya kaunti hiyo na wadau mbali mbali kufanya uhamasisho huo utakaowawezesha wakazi kujua madhara ya ukeketaji.
“Tafadhali ninawaomba kina mama na wazee wetu tusaidiane kumaliza ukeketaji wa wasichana wetu.”Amesema Wangui Ngirici
Leave a Comment