News/Habari

EMBU: Safari ya kufikia haki ya Kaka wawili waliofia mikononi mwa polisi

Hafla ya mazishi ya kaka wawili waliofia mikononi mwa polisi kaunti ya Embu.
Written by admin

Maafisa sita wa polisi wanaohusishwa na vifo vya ndugu wawili kule Embu wamekamatwa na kupelekwa Nairobi.

Sita hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baadaye hii leo kulingana na DCC wa Embu Kaskazini Jeremiah Tumo.

Kukamatwa kwao kunajiri saa chache baada ya DPP Noordin Haji kuagiza wote watiwe mbaroni na kushtakiwa.

Hapo awali walikuwa wamesimamishwa kazi wakati ambapo IPOA nayo ilipendekeza washtakiwe kwa hatia ya mauaji na utelekezaji kazini.

About the author

admin

Leave a Comment