News/Habari

GACHUGU: VIJANA CHUMENI MITANDAONI

Mkurugenzi wa Ajira Digital Dkt. Ehud Gachugu akihutubia warsha ya vijana mjini Nakuru mnamo Septemba 24,2021 alipowataka kukumbatia mpango wa Ajira Digital
Written by admin

Mkurugenzi wa mpango wa utoaji mafunzo na ajira maarufu kama Ajira Digital dkt Ehud Gachugu, ametoa wito kwa vijana kuendelea kujisajili kupata mafunzo ya kidigitali ambayo yatawahakikishia ajira kupitia matumizi ya mitandao.

Akizungumza na wanahabari hapa mjini Nakuru, dkt Gachugu ambaye pia anasimamia ajira kwenye muungano wa sekta za kibinafsi KEPSA, amesema tangia kuzinduliwa kwa mpango huo mwaka wa 2016, zaidi ya vijana milioni moja wamekuwa wakipewa mafunzo kila mwaka kuhusu namna ya kujiajiri kupitia mitandao.

“Mpango wa Ajira Digital  unalenga kuwasaidia vijana wasiopungua milioni moja kila mwaka kwa kuwapa mafunzo ya kidijitali, hivyo wanaweza kujiajiri na kuendeleza biashara zao katika ulimwengu wa kidijitali” amesema Gachugu.

Kulingana na Gachugu, wafadhili wanazidi kujitokeza kusaidia  vijana  kupitia Ajira Digital haswa wakati huu wa covid-9, lakini lazima vijana wajitolee kusaidiwa. Kulingana na mkurugenzi huyo, uwekezaji pia unahitaji msukumo wa kidigitali kuwezesha vijana kuuza bidhaa na huduma zao mitandaoni pia.

“Mpango huu wa Ajira Digital pia unalenga kuafikia Ruwaza ya mwaka wa 2030 kwa kuhakikisha Kenya inakumbatia matumizi, ubunifu na ukuaji wa teknolojia kwenye sekta mbali mbali” ameongeza Gachugu

About the author

admin

Leave a Comment