Gavana wa Uasin Gishu Jackson Mandago ametoa onyo kwa wale ambao wanakwepa kulipia kodi za ardhi akisema kuwa watachukuliwa hatua.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa hamasisho la umma kuhusu umuhimu wa kulipa kodi katika makao makuu ya kaunti hiyo, Mandago amewasihi wakaazi wa kaunti hiyo kuwajibika ili kuinua kaunti hiyo kiuchumi.
Amesema kuwa, fedha ambazo serikali za kaunti zinapokea kutoka kwa kodi, itaamua kiwango cha fedha ambazo zinapokea kutoka serikali kuu. Kwa hivyo, amewasihi wamiliki wa ardhi kufwata sheria hiyo kwa manufaa ya wakaazi wa eneo hilo kupitia kwa maendeleo ya kaunti hiyo. Serikali ya kaunti hiyo inanuia kukusanya shilingi bilioni 1.2 mwaka huu kutoka kwa kodi za ardhi.
Serikali ya Kaunti ya Uasin Gishu imefanya mkutano wa mashauriano na wafanyabiashara wa kaunti hiyo ya kutafuta suluhu kuhusiana na malalamishi yao.
Wakati wa mkutano huo ulioongozwa na mbunge wa Kapseret Oscar Sudi na baadhi ya mawaziri wa kaunti hiyo serikali ya Kaunti hiyo na wanabiashara wamekubali kuendelea kushirikisha uhusiano bora wa kufanya kazi na utaratibu wa utatuzi wa migogoro juu ya maswala yanayoathiri wafanyabiashara wadogo.
Vilevile mwakilishi wadi wa huruma Francis Muya amewataka wanabiashara hao kutoingiza siasa swala hilo akisema kuwa gavana Jackson Mandago na mawaziri wake hawausiki vyovyote na madai hayo.
Leave a Comment