News

Gharama ya kurudi shule yawatatiza wazazi

Written by admin

    

Huku shule zikitarajiwa kufunguliwa Jumatatu ijayo kwa muhula wa kwanza  mwaka huu wa 2020, maduka ya uuzaji sare za shule na vitabu kwenye vituo vya kibiashara mbali mbali hapa Nakuru, yanaendelea kushuhudia msongamano mkubwa.

Baadhi ya wazazi waliozungumza na kituo hiki kutoka Rongai wameeleza kukabiliwa na ugumu wa kununua sare hizo mapema kutokana na ukosefu wa fedha na gharama kubwa ya kimaisha, ikizingatiwa sherehe za Krisimasi na mwaka mpya.

 Wameitaka serikali kuhakikisha kuwa vitabu vya mtaala mpya wa CBC vinapatikana madukani.

About the author

admin

Leave a Comment