‘Hakimu’ bandia Victor Kiprop Ng’eno atasalia korokoroni kwa wiki nyingine moja kabla ya mahakama kutoa uamuzi wa ombi lake la kuachiliwa kwa dhamama.
Ng’eno na mkewe Mercy Chepkurui walifikishwa mbele ya hakimu mkuu Isaac Orengo mnamo Jumanne kwa kosa la kujifanya wafanyikazi wa idara ya mahakama, ambapo waliwalaghai wakenya mamilioni ya fedha.
Wawili hao walikanusha mashtaka hayo na kuomba mahakama kuwaachilia kwa dhamana.
Hata hivyo upande wa mashtaka kupitia Monica Mburu ulipinga ombi hilo kwa misingi kuwa mshtakiwa anaeza kutoroka ikizingatiwa uzito wa kesi yake, na wala haijulikani anakoishi rasmi.
Ng’eno anadaiwa kulaghai watu kadhaa shilingi milioni tano kati ya Oktoba Mosi 2018 na Disemba 2019.
Hata hivyo mkewe Mercy Chepkurui aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi 350,000 baada ya upande wa mashtaka kusema hauna sababu za kuendelea kumzuilia zaidi. Kesi hiyo itatajwa Novemba 2 mwaka huu.
Mwandishi, Sarah Nyangeri Chege
Leave a Comment