Hatua ya serikali kupunguza bajeti ya idara mahakama itasitisha mipango ya ujenzi ambayo ilikuwa imeratibiwa na idara hiyo.
Wakazi wa Molo wamesema ujenzi wa gereza katika eneo la Molo ambao uliahidiwa na jaji mkuu David Maraga huenda ukakosa kutimia huku serikali kuu na idara ya mahakama zikiendelea kuzozana kuhusu ugavi wa fedha za bajeti.
Wakazi wamesema iwapo ujenzi huo utafaulu utapunguza msongomano wa wafungwa katika gereza la Nakuru.
“Hawa watu wenye kufungwa ni watoto wetu,na jela ni mahali kama nyumba tu pa kuishi ,huu mzozo unafaa kuisha ili ujenzi wa jela ukamilike.” Mmoja wa mkaazi asema.BERNARD WAWERU
Leave a Comment