News/Habari

Justine Wamae agura chama chama cha roots

wamae asonga mbele
Written by admin

Aliyekuwa muwaniaji mwenza wa chama cha Roots Justina Wamae, ametangaza kuwa amekigura chama hicho kinachoongozwa na aliyekuwa muwaniaji wake wa Urais Prof. George Wajackoyah.

Uhusiano wa viongozi hao wawili umekumbwa na utata baada ya kutangazwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa tarehe tisa mwezi Agosti mwaka 2022.

Kupitia mtandao wake wa Twitter, Justina ambaye alitangaza kumuunga mkono Rais Dkt. William Ruto, alisema ameondoka katika chama hicho, huku akiwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa msajili wa vyama vya kisiasa Ann Nderitu ili hatua zichukuliwe.

Kwa upande wake msajili wa vyama vya kisiasa katika kupokea barua ya Justina aliondoa jina lake katika sajili ya chama cha Roots.

Masaibu ya Justina katika chama hicho yalizidi kuongezeka baada ya hapo awali kukaidi maagizo ya mkubwa wake ya kujiuzulu, kwa kukosa kuzingatia katiba na manifesto za chama hicho.

Kamati ya nidhamu  ya chama hicho ilikuwa imetishia kuchua hatua za kinidhamu dhidi ya Justina kutokana na matamshi ambayo ilidai hayaambatani na sera za chama hilo.

Aidha tarehe 30 mwezi Agosti mwaka huu, kiongozi wa chama hicho George Wajackoyah alimsimamisha kazi naibu wake na mahala pake kumpa mtu mwingine.

Katika kile alichokitaja kuwa mabadiliko katika chama hicho, Wajackoyah alitangaza orodha ya maafisa wapya na nyadhifa zao, huku akimtaja Vinod Ramji kuwa naibu wake.

Awali washirika wa justina wamae walikuwa wamesistiza kutojiuliza kwake

About the author

admin

Leave a Comment