Chama cha Kanu sasa kimetoa changamoto kwa maafisa wa usalama kumsaka aliko kiongozi wa vijana wa cha hicho Billian Ojiwa aliyetoweka Jumapili jioni.
Kulingana na mkewe Nerima Wako, juhudi za kumfikia Ojiwa zimekuwa zikiambulia patupu kwani hapatikani kwa simu.
Kupotea kwa Ojiwa kunajiri takriban wiki moja baada ya mwanaharakati Caroline Mwatha kupotea kwa njia tatanishi nyumbani kwake Dandora kaunti ya Nairobi.