Gavana wa kaunti ya Nakuru Susan Kihika na balozi wa taifa la Uholanzi nchini Kenya (Maarten Brouwer) wanatarajia kuzindua hazina ya vijana itakayowawezesha kufanya biashara kama njia moja ya kufadhili utoaji ajira kwa vijana wakati wowote kuanzia sasa.
Aidha kulingana na waandalizi wa hafla hiyo wanadai kwamba gavana kihika pamoja na washikadau mbalimbali walifikia leongo hilo ilikupunguza asilimia ambayo inaendelea kupanda nchini ya vijana kukosa ajira.
Hata hivyo mpango huo utahusisha sekta ya kibinafsi kwani wanaamini kuwa kuna pengo ambalo sekta hiyo itajaza katika kutekeleza jukumu hilo ili kuwafaidi vijana kutoka sehemu mbalimbali.
Leave a Comment