News/Habari

KENYA: Arubaine Za Mlanguzi

Written by admin

Idara ya kukabiliana na makosa ya jinai nchini imemkamata mwanammke mmoja kwa jina Beatrice Awuor, na kupata vidonge vilivyofungiwa dawa ya kulevya aina ya Heroin.

Mshukiwa Awuor (42), alipatikana na vidonge 60 vinavyoaminika alikuwa anajitayarisha kuvimeza ili aweze kusafirisha dawa hiyo hadi maeneo yasiyojulikana.

Makachero wa kupambana na mihadarati walifanikiwa kumkamata mshukiwa katika eneo la Nasra mtaani  Kayole  kaunti ya Nairobi baada ya kupashwa habari kuhusu mama huyo mlanguzi wa dawa za kulevya.

Makachero hao walipata hati yake ya usafiri pamoja na za wengine wawili zilizo na majina ya  Caroline Adongo Mujibi  na  Risper Auma Ochieng, ambao wanashukiwa kuwa washirika wake.

Pia walipata kitambulisho cha kazi ambacho kilimtambulisha kama nesi kwenye hospitali ya Mbagathi.

Wakati hayo yakijiri, idara ya upelelezi wa jinai nchini imewaomba wakenya kutambua washukiwa kadhaa walionaswa kwenye video inayosambaa mitandaoni, wakimpiga kitutu mwenzao ambaye alichukua video ya kufichua namna wamekuwa wakiendeleza biashara ya utengenezaji pesa bandia maarufu kama Wash Wash.

About the author

admin

Leave a Comment