Kenya imepokea shehena la pili la dozi 210,000 za Pfizer kutoka kwa serikali ya Marekani katika mkakati wa kuwezesha juhudi za kukabiliana na virusi vya Corona.
Chanjo hizo zimewasili katika uga wa JKIA mwendo wa saa saba asubuhi ya kuamkia leo kutoka kituo cha usambazaji corona cha COVAX.
Hii inajiri wiki mbili tu baada ya Kenya kupokea chanjo zingine 795,600 aina ya Pfizer-Biontech pia.
Shehena nyingine inatarajiwa nchini wiki chache zijazo ili kuafikia dozi milioni 2.03 aina ya Pfizer ambazo serikali ya Marekani iliahidi Kenya.
Leave a Comment