Rais Uhuru Kenyatta amewateua rasmi makamishna wanne wapya wa tume ya mipaka na uchaguzi nchini (IEBC).
Rais Kenyatta amewateua Juliana Whonge Cherera, Francis Mathenge Wanderi, Irene Cherop Masit na Justus Obonyo Nyang’aya baada ya bunge la kitaifa kupitisha majina yao jana, Jumatano.
Majina ya wanne hao yamechapishwa kwenye gazeti la serikali na wanatarajiwa kula kiapo, leo Alhamisi.
Wanne hao watahudumu kwa kipindi cha miaka sita.
Hatua hiyo inamaanisha kuwa kwa sasa IEBC imetimiza idadi ya makamishna wanaohitajika kikatiba.
Kwingineko rais pia ameteua makamishna watano wa tume ya kuajiri waalimu nchini (TSC) na kumaliza shida iliyokuwepo.
Rais ameteua Nicodemus Ojuma Anyang, Christine Kahindi, Anneta Wafukho na Salesa Adano, na Sharon Chelagat kujiunga na TSC kwa kipindi cha miaka sita.
Leave a Comment