Serikali ya Kenya inafanya kila jitihada kuwaondoa Wakenya tisa ambao wamekwama nchini Afghanistan baada ya nchi hiyo kutekwa na kundi la Taliban.
Wapiganaji wa kundi la Taliban waliteka miji muhimu nchini humo na kutwaa serikali ya nchi hiyo punde tu baada ya Amerika kuondoa majeshi yake na kutamatisha uwepo wao wa miaka 20.
Wizara ya Mambo ya nje inasema kwamba inashauriana na ubalozi wa Kenya mjini Islamabad, Pakistan, kukusanya maelezo muhimu kuhusu Wakenya wote ambao huenda wamekwama nchini Afganistan.
Leave a Comment