Kituo cha polisi cha Gathoge katika kaunti ndogo ya Gichugu kule Kirinyaga kimefungwa kwa muda wa siku 10 baada ya mmoja wa maafisa wake kupatikana na virusi vya corona.
Akizungumza asubuhi ya leo, kamanda wa polisi kaunti ya Kirinyaga Leah Kithei amesema maafisa watano kutoka kituo hicho wamewekwa karatini ilhali mmoja amelazwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Kianyaga.
Wenyeji wa eneo hilo wametakiwa kutafuta usaidizi katika kituo cha polisi cha Kutus endapo wanahitaji msaada wa polisi kutoka kituo hicho cha Gachoge.
Kituo hicho tayari kimepuuliziwa dawa na maafisa wa afya eneo hilo.
Leave a Comment