Hali ya mshangao iliibuka maeneo ya
Bonchari baada ya genge la wezi kuvamia kanisa la Gesonso SDA na kuiba
mali ya kanisa yenye dhamani kubwa isiyojulikana.
Shemasi Simon Mogusu amesema kuwa
washirika wa kanisa hilo walipigwa na butwaa baada ya kufika kanisani na kupata
kuwa viti na vyombo vinavyotumika katika ibada ya ushirika mtakatifu
havikuwepo.
“Tulipata kuwa zaidi ya
viti 150, sinia na vikombe vinavyotumika wakati wa ushirika mtakatifu
havikuwepo pale kanisani” Mogusu alisema.
Kiongozi huyo wa kanisa alisema
kwamba sinia na vikombe vya ushirika mtakatifu haviwezi kutumika manyumbani na
kuagiza waliochukua kuzirejesha kanisani.
Mogusu ametoa ombi kwa maafisa wa polisi kufanya haraka katika upelelezi kuhusiana na wizi huo kwani waumini wanatazamia kurejelea ibada zao za kawaida kanisani siku ya Jumamosi baada serikali kuruhusu kanisa zilizokuwa zimefungwa maeneo hayo kufunguliwa. You can often find https://parkirpintar.com/pet-friendly-casinos-in-las-vegas-nv/ the bonus codes from terms and conditions although they might be called promo codes.
Kesi hiyo iliripotiwa katika kituo
cha polisi cha Gesonso na upelelezi kung’oa nanga.
Leave a Comment