Muungano mwingine wa kisiasa unaelekea kuundwa kwa jina National Alliance for Change.
Muungano huo unawaleta pamoja spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi, gavana wa Makueni Kivutha Kibwana, na aliyekuwa katibu wa maendeleo ya biashara kwenye kongamano la umoja wa mataifa Mukhisa Kituyi.
Hapo jana, Jumanne, watatu hao walifanya mkutano wa saa tatu jijii Nairobi, ambapo baadaye walieleza kwamba wanalenga kubadilisha siasa za Kenya zinazoandamwa na mgawiko na machafuko mara nyingi.
Muungano wao unajiri wakati ambapo ODM na Jubilee wapo kwenye mazungumzo ya kufanya kazi pamoja, navyo vyama vya Wiper, Kanu, Anc na FORD Kenya zikibuni muungano wa O.K.A
Leave a Comment