Hali ya watu kushiriki ngono bila kinga imechangia kwa aslimia themanini, ya visa vinavyosajiliwa nchini vya virusi vya HIV. Hayo yamesemwa dkt. Michael Odeka kutoka shirika la Impact Health Care International.
Akizungumza kwenye kituo hiki asubuhi leo, Odeka amesema aslimia tano ya visa hivyo, huchangiwa na watoto kuambukizwa kutoka kwa mama mja mzito, wakati wa kuzaliwa au wakati wa kunyonyesha.
Dkt. Odeka wakati uo huo amesema unyanyapaa ni tatizo kubwa katika kuwahakikishia wenye virusi hivyo afya bora.
Shirika hilo limeshauri vijana ambao hawajafikia umri wa kuingia kwenye ndoa kujiepusha na ngono, na walio oa kuwa na uaminifu kwenye ndoa zao.
Leave a Comment