Afisa mmoja wa polisi anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kabati, Murang’a kwa madai ya kumuibia dereva wa TukTuk shilingi 1,100.
Kulingana na DCI, polisi huyo alikamatwa baada ya dereva wa TukTuk kupiga ripoti kuhusu tukio hilo ambalo linadaiwa kufanyika mnamo Jumanne jioni.
Dereva huyo anadai kuwa mshukiwa alisimamisha TukTuk yake na kumwagiza atoe hongo ya shilingi 2000,na kukataa kutii agizo hilo, polisi huyo anaripotiwa kunyakua shilingi 300 alizokuwa ameshika kwa mkono.
Pia inasemekana kuwa afisa huyo alikagua mifuko ya jamaa huyo na kupora kiasi cha shilingi 800 alizokuwa nazo, tukio lililoacha suruali ya mhasiriwa ikiwa imeraruka vipande vipande.
Polisi huyo kwa sasa anazuiliwa huku uchunguzi zaidi ukiendelea ili kuhakikisha haki imetendeka.
Leave a Comment