Ukavu unatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi kulingana na idara ya utabiri wa hali anga nchini.
Kwa mujibu wa idara hiyo,kaunti 21 zitapokea mvua chache sana.
Kaunti hizo ni pamoja na West Pokot, Kitale, Eldoret, Kakamega, Bungoma, Nakuru, Naivasha, Kericho, Nyamira, Kisii, Bomet na Molo.
Zingine ni Kabarnet, Eldama Ravine, Laikipia, Nyandarua, Nanyuki, Nyeri, Meru, Tharaka na Samburu.
Hata hivyo maeneo ya Maralal , Narok na Turkana yatapokea mvua. Idara hiyo imetoa wito kwa wakulima kutumia mvua itakayonyesha vizuri kwa manufaa yao.
Leave a Comment