News/Habari

Kenya: Utamu utamu kwa wabunge

Bunge la Kenya.
Written by admin

Notisi kwenye gazeti rasmi la serikali iliowekwa na IEBC kuhusu matumizi ya pesa ni haramu, na wabunge sasa wamejitangaza huru kutumia kiasi cha pesa ambacho wanataka katika uchaguzi mkuu ujao.

Hili liliamuliwa na kamati ya bunge kuhusu sheria (Committee on Delegated Legislation) saa chache baada ya tume ya IEBC kukiri kwamba ilifanya makosa wakati wamefika mbele ya kamati hyo asubuhi ya leo.

Kulingana na wabunge, sheria yoyote inayozuia matumizi ya pesa ilifaa kuwasilishwa na kupitishwa na bunge miezi 12 kabla ya uchaguzi, na hivyo notisi hiyo ya tarehe 9 ilikuwa imechelewa wakati IEBC imeshikilia kwamba kisheria uchaguzi ni wa tarehe 9 agosti mwaka ujao.

Wabunge wanasema notisi hiyo inakwenda kinyume na sheria ya ufadhili wa kampeni za kisiasa mwaka wa 2013.

Wakuu wa IEBC walikuwa wamekutana na kamati hiyo asubuhi ya leo, Jumatano , wakiongozwa na mwenyekiti wake Wafula Chebukati katika majengo ya bunge.

About the author

admin

Leave a Comment