Watahiniwa wa mtihani wa KCSE 2020 wanatarajiwa hii leo kujua vyuo vikuu watakavyojiunga navyo pamoja na kozi watakazofanya.
Watahiniwa 747, 161 walifanya mtihani huo mwaka huu huku wanafunzi 143, 140 wakifikisha alama ya C+ inayohitajika ili kuhitimu kuingia chuo kikuu kwa ufadhili wa serikali.
Idadi hiyo imeongezeka kwani mwaka wa 2019 ni wanafunzi 125, 746 pekee ambao walihitimu, Mwaka uliopita vyuo vikuu vya umma vilichukua watahiniwa 108,378 ambao walikalia mtihani mwaka wa 2019 huku 17,368 wakichukuliwa katika vyuo vikuu vya kibinafsi. Nafasi 100,000 zimetengewa watahiniwa hao katika vyuo vya kiufundi kupata mafunzo ya diploma na cheti.
Leave a Comment