News/Habari

KENYA: Wazazi wakamatwa kisa wanao kukosekana shuleni.

Written by admin

Wazazi 47 wamekamatwa katika kaunti ya Kwale   kwa kukosa kupeleka watoto wao shuleni.

Kamishna wa kaunti ya Kwale  Joseph Kanyiri, alisema kuwa wazazi hao walikamatwa kutoka sehemu mbali mbali za kaunti hiyo baada ya kushindwa kueleza walipo wanao.

Eneo bunge la Kinango linaongoza kwa idadi ya watoto ambao hawakujiunga na kidato cha kwanza huku wazazi 18 kutoka huko wakikamatwa.

Operesheni hiyo ilifanywa na manaibu kamishna, machifu, wazee wa kijiji, polisi na  wakuu wa shule.

About the author

admin

Leave a Comment