News/Habari

KENYA: WENGI WAPUUZA UZAZI WA MPANGO

Written by admin

Matumizi ya mbinu za kupanga uzazi miongoni mwa wanawake yamepungua hapa nchini, Kenya, kutokana na athari za janga la COVID-19.

Kaimu mkurugenzi wa maswala ya afya nchini Dkt. Patrick Amoth, amesema kuwa matumizi ya mbinu hizo yamepungua kutoka asilimia 44% katika mwaka wa 2019/2020 hadi asilimia 29.6% katika mwaka wa 2020/2021.

Katika taarifa wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya matumizi ya mbinu za kupanga uzazi, Amoth alisema kuwa wizara ya afya inalenga kupanua upatikanaji na matumizi ya mbinu za kupuanga uzazi wakati huu wa kipindi cha janga la COVID-19 ili kuzuia mimba zisizokusudiwa.

Dkt. Amoth ambaye alikuwa akiongea wakati wa kikao chake cha kila wiki katika mtandao wa Twitter kwa jina Ask the DG alisema kuwa licha ya mpango mkakati zaidi kuhitajika Kenya ni miongoni mwa mataifa yanayoongoza katika matumizi ya mbinu za kisasa za kupanga uzazi barani Afrika.

About the author

admin

Leave a Comment