News/Habari

KERICHO: Mama arithishwa kifo cha mwanae

Written by admin

Huzuni imetanda katika kijiji cha Chepkosilen  kule 
Belgut kaunti ya Kericho baada ya mwanamme mmoja kumuua mamake kwa
kumdunga kisu kutokana na mzozo wa shamba.

Akidhibitisha hayo, naibu chifu  David Mutai alisema mshukiwa Wesley Mutai, alimdunga mama yake,  Sarah Sang, mwenye umri wa miaka 65 kwa kisu baada ya kuwapata wakipigana na kaka yake mkubwa na kujaribu kuwarai waache vita. If you prefer to play a game https://clickmiamibeach.com/ in flash mode you can use a compatible flash player such as Oracle Flash Player (Beta).

Afisa huyo wa utawala anasema mzozo ulizuka baada ya mshukiwa Wesley kumlaumu kaka yake mkubwa Richard Mutai kwa kuingilia sehemu ya ardhi aliyogawiwa.

Mama huyo alidungwa kisu kifuani na kuaga dunia papo hapo, na kisha mshukiwa
akajaribu kutoroka ila akakamatwa na wananchi na kupelekwa kituo cha polisi cha
Kabianga.

Mwili wa mama huyo upo kwenye makafani ya hospitali ya Siloam.

About the author

admin

Leave a Comment