News/Habari

Kiambu: Kifo cha Laki moja unusu

Gari lililoharibika kisa ajali
Written by admin

Dereva mmoja alitozwa faini ya shilingi 150,000 na mahakama ya Kiambu kwa kuendesha gari vibaya na kusababisha kifo cha mtu mmoja.

Lucas Thuo Ngethe alikabiliwa na mashtaka ya kugonga Michael Njoroge King’ang’i  mnamo Juni 20 mida ya saa kumi na mbili jioni katika barabara ya kutoka Kanunga kuelekea Kiratina, kaunti ya Kiambu.

Baada ya kusababisha ajali hiyo Ngethe anadaiwa kuendelea na safari yake mbio na kutoweka.

Ngethe alitafutwa na kupatikana siku 10 baadae baada ya mhasiriwa aliyegonga kuangamia kutokana na majeraha mabaya aliyopata mwilini.

Njoroge aliaga alipokuwa anapokea matibabu katika hospitali ya Kiambu Level 5.

Hata hivyo Ngethe hakukanusha mashtaka dhidi yake. Hakimu mkuu katika mahakama ya Kiambu Grace Omodho aliamuru Ngethe ahudumu kifungo cha miaka mitatu.

Mwendesha mashtaka Viola Muthoni aliambia mahakama kuwa Ngethe alikosa kusimama baada ya kusababisha ajali.

Kwa upande wake Ngethe alijitetea kwa kusema kwamba  alihofia kuwa angechomwa na watu wenye ghadhabu walioshuhudia ajali hiyo.

Polisi walimkamata Ngethe baada ya kifo cha Njoroge kilichotokana na  majeraha mabaya mwilini.

About the author

admin

Leave a Comment