Wakulima wa viazi kutoka eneo la Bonde la Ufa wamelalamikia kushuka kwa bei ya zao hilo kutoka Sh 1,500 hadi Sh700.
Mwenyekiti wa chama cha wakulima hao nchini, Joshua Ng’eno, alisema kuwa bei hizo zimeshuka kwa kiasi kikubwa huku madalali pia wakiwapunja kwa kurefusha magunia kwa kuongeza kilo 20 zaidi.
Ng’eno alitoa changamoto kwa maafisa wa usalama kuwanasa madalali wanaokiuka sheria ya upakiaji wa viazi.
Wakati uo huo wakulima sasa wanaitaka serikali kuwekeza katika barabara za mashinani ili kuwawezesha kufikisha mazao yao sokoni kwa muda ufaao na kuzuia mazao kuoza kwa kushindwa kuyasafirisha hadi sokoni kwa kutumia barabara mbovu.
Leave a Comment