Maafisa wa DCI katika kaunti ndogo ya Nyakach kule Kisumu wanachunguza kisa ambapo mtoto mvulana wa siku nane amefariki katika kile kinasemekana ni kufeli kwa zoezi la kumpasha tohara mtoto huyo katika Kanisa la Nomiya.
Wazazi wa mtoto huyo pamoja na kiongozi wa kanisa aliyefanya tohara hiyo, wameandikisha taarifa katika kituo cha polisi cha Nyakach.
Kisanga hicho kilitokea katika kijiji cha Kaloo kulingana na chifu wa lokesheni ya Sigoti Michael Sati, ambaye pia alisema familia hiyo iliharakisha kumzika mtoto huyo siku iyo hiyo aliyoaga.
Chifu huyo alisema mtoto huyo alizikwa pasi na wazazi wake kujulisha utawala kuhusu kifo chake.
Leave a Comment