News/Habari

KIUNJURI: Mlima Kenya lazima muukwee kwa mikakati!

Aliyekuwa waziri wa kilimo Mwangi Kiunjuri.
Written by admin

Aliyekuwa waziri wa kilimo Mwangi Kiunjiri amewaonya wagombea urais katika uchaguzi mkuu ujao kuwa hakuna yeyote anastahili kujihakikishia uungwaji mkono wa aslimia 100 wa wakaazi wa mlima kenya.

Bila kutaja yeyote, Kiunjuri alisema lazima wanasiasa waendelee kuomba uungwaji mkono kutoka mlima Kenya kwa kuwaambia nini watawafanyia wakenya, ila sio kujigamba kwamba wana ufuasi eneo hilo lenye wingi wa kura baada ya ziara chache.

About the author

admin

Leave a Comment